Majibu ya Mwanamuziki Bob Haisa Kuwa Mwehu, Kuachana na Mkewe


Msanii wa muziki wa mduara Bob Haisa, amesema kuna muda watu walikuwa wanamshangaa badala ya kumpa ushirikiano, wengine walimuona amepoteza ramani na dira ya maisha huku wengine walimsema kwamba amekuwa mwehu.

Taarifa hizo zimekuja baada ya kuachana na aliyekuwa mke wake kipindi cha miaka 10 iliyopita, sasa kupitia EATV & EA Radio Digital, msanii huyo amenyoosha maelezo kuhusu tuhuma za yeye kuwa mwehu.

"Nimechana na mke wangu  na kumpa talaka moja miaka 10 iliyopita, lakini watu wamekuja kujua na kulizungumzia tukio hilo sasa hivi, sababu za kuachana naye ilikuwa ni riziki imekwisha na mapenzi hakuna ila hatujakoseana, japo kuna wengine walisema nimepoteza ramani na dira huku wengine wakisema kwamba nimekuwa mwehu " amesema Bob Haisa.

Aidha ameongeza kusema "Kwenye maisha yangu sijawahi kuwa chizi labda uchizi wangu upo kwenye harakati, ujue mtu akija na akili iliyokuzidi upeo wako huna cha kumuita zaidi ya kumwambia mjinga au mwehu"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad