Wachuuzi wa ngono katika kaunti ya Vihiga Kenya sasa wanautaka usimamizi wa kaunti hiyo kuwapa misaada ili kujikimu wakati huu mgumu wa kiuchumu kufuatia marufuku ya kutotoka nje nyakati za usiku.
Chama cha Makahaba nchini waanzisha mchango wa kuwasaidia wahudumu wa afya
Makahaba hao ambao kwa sasa hawawezi kuuzia wanaume vitumbua vya nyama mbichi wanadai kukabiliwa na changamoto za kifedha kutokana na janga la corona. Warembo hao ambao biashara yao hunoga gizani kwa sasa wamefungiwa kitega uchumi chao kutokanna masharti ya kutotoka nje usiku.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao kaunti ya Vihiga Janet Minayo almaarufu ‘Take Away’na katibu wake Kitagwa Ondisa, walisema kuwa tangu kuzuka kwa janga la covid 19 hali ya biashara yao imekumbwa na ukosefu mkubwa wa wateja ambao hurudi nyumbani mapema.
Hakuna biashara ya ngono tena! Makahaba 24 wapelekwa karantini ya lazima
Mama Take Away ametowa wito kwa kaunti hiyo kuzingatia changamoto zao msimu huu, ikiwemo kuwataka maafisa wa usalama eneo hilo kuwaruhusu kuendesha biashara zao ili kukimu na mahitaji yao.