Makosa Makubwa Tunayofanya Wanaume Katika Mapenzi

NAWAPA KISA KIFUPI TUU AMBACHO KINANISIBU KWA SASA,

Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume). Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially akina mama.

Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).

Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.

Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.

Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.

Najua fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake. Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?

READ MORE:

Hii Hapa Sababu Kubwa Inayowafanya Wanawake Kupiga Kelele Wakati wa Tendo la Ndoa

Madhara ya kufanya Mapenzi kinyume na Maumbile

Kutana na Binti Anayekunywa Mkojo Kila Siku ili Kutunza Ngozi yake

Huddah Monroe "Sijafanya Mapenzi Kwa Siku 60"



Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kaka pole kwa huu mkasa,cha msing kuwa mwaminifu ktk ndoa matatizo co7bu ya kumwendea kinyume mwenzako,km unamawasiliano na huyo mme wke na unania ya kumsaidia tafuta njia sahih ya kumpa tarifa za familia yke huyo kaka.

    ReplyDelete
  2. hakuna haja ya kuwa naye kimapenzi tamini ndoa yako na familia yako,mwambie kuwa hauko tiali kwani ulikuwa unamsaidia siyo kukupa zawadi ya ngono,bali mungu ndo atakayekupa zawadi kwa msaada wako.kama wewe ni mwepesi wa matamanio ya kungonoka ndo hivyo tena jibu unalo

    ReplyDelete
  3. pole sana ndugu yetu. Ukweli ni kwamba hawa ndugu zetu ukiwafanyia fadhila wao wanatamani kulipa kwa njia ya ngono nashukuru hii mada imekuja wakati muafaka kwani na sisi wengine tunakumbwa na tatizo kama lako. Ila chakufanya we mwambie tu unashukuru kwa hiyo fadhila alafu potezea ila najua kwa upande wake hato jisikia vizuri kwa alikuwa ameazimia kufanya hivyo. Pia ukae makini kwani anaweza kukugeuka na kumwambia mme wake kuwa we ndiye uliyekuwa unamtaka kimapenzi. Kwa kukataa kwako. Nakupa tena pole ndugu na usichoke kumsaidia huyo mke wa ndugu yako. Kwani utalipwa na mungu.

    ReplyDelete
  4. pole sana huo ndio uanaume

    ReplyDelete
  5. pole sana ndugu kaza moyo acha kutenda tofauti thamin ndoa yako kuwa mwaminifu huyo anata akulagai na ngono ili aweanapata msaada kwa ukaribu so be care braza

    ReplyDelete
  6. pole sana ndugu kaza moyo acha kutenda tofauti thamin ndoa yako kuwa mwaminifu huyo anata akulagai na ngono ili aweanapata msaada kwa ukaribu so be care braza

    ReplyDelete
  7. pole sana ndugu kaza moyo acha kutenda tofauti thamin ndoa yako kuwa mwaminifu huyo anata akulagai na ngono ili aweanapata msaada kwa ukaribu so be care braza

    ReplyDelete
  8. pole sana ndugu kaza moyo acha kutenda tofauti thamin ndoa yako kuwa mwaminifu huyo anata akulagai na ngono ili aweanapata msaada kwa ukaribu so be care braza

    ReplyDelete
  9. pole sana ndugu kaza moyo acha kutenda tofauti thamin ndoa yako kuwa mwaminifu huyo anata akulagai na ngono ili aweanapata msaada kwa ukaribu so be care braza

    ReplyDelete
  10. Huwezi recover ten a pesa zako,so Chanachana hiyo mauchi fasta,,,

    ReplyDelete
  11. Ni kweli lakini mara kwa mara kuna wanawake wenye tabia ya kumtamani mwanamme mwingine nje ya ndoa hata kama si mkopo na mkopo inaweza ikawa njia ya kupitia na mwanamke wa aina hiyo bwana ake akitoka anatumia pesa kutongozea wanaume hivyo kinachotakiwa pamoja na yote hata sisis wanaume tunapooa basi tusikurupuke tu bila kujuana tabia mara nyimgi mtu hukua na tabia yake tangu anapobarehe ni mara chache sana tabia za kuiga mtu kukua nazo

    ReplyDelete
  12. Everybody is responsible for his/her own actions,Stay away from her,ukimgusa tu na wewe utaisahau familia yako kama mume wake alivyomsahau yeye,na kwa kuwa anajua wife wako yuko mbali atahamia kwako kabisaaaaaaaa.Ingawa ukweli unauma lkn mwambie ukweli kuwa humuhitaji kimapenzi ule ni ulikuwa ni msaada tu,akiendelea mwambie utamripot kwa mume wake.But haya yote ni kama umedhamiria kutomduu.

    ReplyDelete
  13. kijana ulishafanya yako ya kiubinadamu na ukamsaidia kama binadamu mwenzako tena mke wa rafiki yako. hayo mengine achana nayooo mke wa mtu ni sumu. hizo pesa makaratasi hasara rohooo sasa kma unataka siku roho yako iondolewe kwa sababu ya mapenzi basi tembea naye huyo mwanamke . so inshort achana na huyooo mwanamke usiwasiliane nae tena. GUBE GUBE HILOOO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad