PAKA wa kufugwa nchini China amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid -19) Idara ya kilimo na uvuvi mjini humo imesema kuwa paka huyo hajaonesha dalili ya ugonjwa huo.
Kwa mujibu iliyotolewa na idara hiyo Machi 31 mwaka huu imeeleza, hadi sasa hakuna uthibitisho kuwa wanyama wa kufugwa wanaweza kuwa chanzo cha virusi hivyo na kuwashauri wamiliki wa mifugo kutotupa mifugo yao.
Machi 31, Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia tovuti yao walieleza kuwa hadi sasa hakuna uthibitisho kuwa mbwa, paka au mnyama yoyote anaweza kusambaza virusi vya Covid -19.
Imeelezwa kuwa sample zilichukuliwa kutoka kwa paka huyo kutoka mdomoni, puani na tumbo alikutwa na virusi hivyo baada ya kuwekwa karantini Machi 30.
Paka huyo amekuwa mnyama wa tatu kukutwa na virusi hivyo akitanguliwa na mbwa wawili waliokutwa na virusi hivyo hapo awali, Mamlaka zimeeleza kuwa wataendelea kuchunguza na kufuatilia.
Madaktari wa wanyama wamesema kuwa kumekuwa na kisa kingine kimoja cha paka kupata virusi hivyo kutoka kwa mmiliki wake nchini Ubelgiji.