No title



Malkia Elizabeth II wa Uingereza amefuta sherehe za siku yake ya kuzaliwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Kulingana na vyombo vya habari nchiniUingereza,Malkia Elizabeth II haitafanya sherehe maalum ya siku yake ya kuzaliwa kwa sababu ya kuenea kwa virusi vya corona.

Malkia huyo wa Uingereza, ambaye atafikisha miaka 94 baadaye mwezi huu, ametaka sherehe zisifanyike kwani haifa kwa wakati huu.

Malkia huyo vilevile ametaka bendera zisipeperushwe juu ya majengo ya serikali kama italeta shida.

Ni mara ya kwanza malkia ametoa ombi kama hilo katika miaka 68 ya utawala wake.

Malkia ana siku mbili za kuzaliwa: siku yake ya kuzaliwa Aprili 21, 1926, wakati ambapo risasi hupigwa angani kwenye kusherehekea  lakini sikukuu rasmi ya umma inaadhimishwa Jumamosi ya pili ya mwezi Juni ambapo hufanyika gwaride.


Gwaride hilo linajumuisha zaidi ya wanajeshi 1,400, farasi 200 na wanamuziki 400 pamoja na Jeshi la anga likifanya maonyesho angani juu ya ikulu ya Buckingham.

Mnamo Aprili 5, malkia alitoa hotuba maalum kwa taifa - akiwa wa tano  katika utawala wake .

Aliziambia nchi na Jumuiya ya Madola kwamba "kwa kujitenga tunawekana salama."

"Tunajua kuwa corona haitatushinda," alisema. "Ikiwa tutabaki umoja na msimamo, basi tutashinda."

"Tutakutana tena," malkia alisema.

Mlipuko wa corona umewauwa zaidi ya watu 158,600, na kuna maambukizi zaidi ya milioni 2.3.

Watu zaidi ya 590,600 wamepona kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad