Mambo 13 MUHIMU Aliyoyaongelea Rais Magufuli Leo Kuhusu Mapambano Dhidi ya Corona


Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa haitatokea hata siku moja Mkoa wa Dar es Salaam, ukafungwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa kuwa ndiyo kitovu cha mapato ya Taifa.

Hayo ameyabainisha leo Aprili 22, 2020, wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi, Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita

==>>Hapo chini ni Baadhi ya Mambo Muhimu aliyoyasema leo

“Nawapongeza viongozi wa Dini na watanzania kwa ujumla kwa kuitikia wito wa kuliombea taifa kwa siku 3 dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, nina amini Mungu wetu ni wahuruma atatusikiliza na siku moja tutalishinda hili gonjwa

“Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuilinda nchi yetu hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya COVID-19, nimekubaliana na hatua mnazoendelea kuzichukua katika kipindi hiki

"Wananchi tuondoe hofu, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona. Niwaombe watu wa mitandao, waache kupotosha kuhusu ugonjwa huu na wananchi pia nawaomba wawapuuze hawa wanaopotosha. IGP upo hapa kawashughulikie hao, ndiyo saizi yako

"Wengine wanatoa mawazo ya kuifunga DSM, hili haliwezekani hii ndiyo center pekee ya mapato, tuendelee kuchukua hatua lakini si ku-lockdown DSM never, kwahiyo ufungie watu Mil.6 ikitokea Mwanza na yenyewe tuifungie, tutafungia watu wangapi

“Hauwezi kuua corona kwa kupuliza dawa kwenye mabasi na mitaani ile unaua mende na wadudu wengine, ila hatujiulizi kwamba labda kupuliza ndio tunaongeza corona, maana DSM imepulizwa dawa tu na kasi ya wagonjwa imeongezeka.

“Baadhi ya Watanzania wanajishonea wenyewe mask, shona mask yako tumia badala ya kutegemea unazouziwa na hujui wanaouza wana dhamira gani?, viwanda vyetu navyo vianze kutengeneza mask, hizi mask za nje narudia tunaweza kuambukizwa corona kwa mask kutoka nje

“Kuna tunaowaweka katarantini ‘Hosteli za Magufuli’ liangaliwe upya hakuna sababu ya Mtu unamuweka pale anakaa siku 14 wakati unamuona hana tatizo, tushughulike na wagonjwa, badala ya kuwakalisha muda mrefu pale wakati hata mtaani atakuta wanaoumwa, tunapoteza rasilimali

"Benki ya Dunia najua wametoa ofa ya nchi zinazosumbuliwa na Corona kukopa pesa, badala ya kukopesha tena, wasamehe madeni kwa nchi hizi, mfano sisi huwa tunalipa karibu Bil 700, watusamehe ili hizi pesa zikatumike kupambana na hili janga


"Nimemteua Katibu Mkuu mpya ili atoe pia na taarifa za wanaopona, sio kwamba ukipata ugonjwa lazima ufe, tuwaondolee hofu wananchi

"Tuanze kushughulikia hata vitu tunavyoletewa kama zawadi visije kutuletea madhara, unapopewa mask lazima ujue aliyetengeneza, aliyesambaza na misingi ya kutuletea tusije kujikuta tunaambukizwa corona kutoka kwenye mask zinazotoka nje

“Tutangaze pia na wanaopona sio wanaokufa tu, inawapa Watu hofu kwamba ukipata corona lazima ufe, kwani Maralia haiui?, na nimegundua baadhi ya wanaopotosha kwenye mitandao wengine sio Watanzania, namba zao ziko nyingine kwenye Nchi za jirani wanawachafua tu Watanzania

“DSM, na Mwanza niliona mabasi yanapulizwa dawa na hasa DSM, hakuna upuliziaji dawa unaoweza kuua corona, ingekuwa pakipulizwa corona wanakufa, Nchi zinazoendelea wangemwagia Nchi zao kwa Ndege na wasingekuwa wanakufa, kule kupuliza dawa ni upuuzi tu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad