Mambo ni moto! Kadi za njano zitaonyeshwa kwa wachezaji watakaotema mate uwanjani wakati ligi zitakaporejea tena baada ya kusimama kwa muda mrefu kutokana na janga la corona, anafichua ofisa wa Fifa.
Serikali ya Uingereza imesema mazungumzo yanaendelea kwa ajili ya Ligi Kuu England kurejea haraka huku wachezaji wakianza kujifua kwa mazoezi.
Na sasa wale wachezaji wenye kawaida ya kutema mate uwanjani wataadhibiwa ili kuepuka kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona, anafichua mwenyekiti wa kamati ya utatibu ya Fifa, Mikel D'Hooghe.
Wakati huo huo, Uefa imetoa Pauni 236.5 milioni kwenda kwenya nchi wanachama wake ambao wameathirika kwa kiwango kikubwa na janga la corona.