MSEMAJI wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji bora Mtanzania katika nafasi ya kiungo licha ya kuwa bado hajaonesha uwezo wake kwa asilimia 100.
Akizungumzia uwezo wa kiungo huyo, Manara alisema kuwa Fei Toto anatakiwa kujitambua nini anahitaji katika maisha yake ya soka, kwa kuwa amejaaliwa kipaji kikubwa kuliko wachezaji wengi wazawa, lakini amekuwa akikwamishwa na vitu vidogo vidogo ambayo anatakiwa kuvifanyia kazi mapema ili kufikia kwenye kilele cha ubora wa asilimia 100.
“Fei Toto ni moja ya kiungo aliyejaaliwa uwezo mkubwa uwanjani, ndiyo maana hata kocha wa zamani wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike alimtabiria kuwa atakuja kufanya makubwa zaidi kweye soka.
“Bado hajatupa alichonacho kwa asilimia 100%, labda anahitajika kujua nini kesho yake ijayo kwenye maisha ya soka, lakini kuhusu kabumbu yupo vizuri na anaweza akafanya lolote akiwa na mpira katika miguu yake,” aliandika Manara kwenye akaunti yake ya Instagram.
Stori: Issa Liponda,Dar es Salaam