Manula "Hakuna Kama Okwi Simba:



KIPA wa Simba, Aishi Manula amesema kuwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Emmanuel Okwi ni mchezaji bora kuwahi kutokea katika klabu hiyo na bado ana nafasi ya kurudi tena na kufanya vizuri kwani pengo lake halijawahi kuzibika.

Manula amesema kila mchezaji ndani ya klabu hiyo ana ubora wake, lakini Okwi ni mchezaji wa kipekee kuwahi kuichezea Simba, kwani alifanya mambo makubwa na kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda wote aliovaa jezi ya timu hiyo.

Okwi alijiunga na Simba kwa mara ya kwanza 2010 akitokea Sc Villa, kisha akatimka 2013 na kwenda Etoile du Sahel, kisha SC Villa, Young Africans, kisha 2014 akarudi tena Simba.

Akaondoka 2017 kwenda SønderjyskE ya Denmark, akaenda Sc Villa na kurudi tena Simba 2017 na 2019, akatua Al Ittihad Alexandria Club ya Misri.

Akizungumzia ishu hiyo Manula alisema: “Pengo la Emmanuel Okwi haliwezi kuzibika kirahisi kwenye kikosi chetu na bado tunahitaji huduma yake. Lakini siyo kwamba waliopo sasa hawana ubora bali kila mchezaji ana ubora wake na ubora wa Okwi ni tofauti na ubora wa mchezaji mwingine yeyote, hivyo hakutatokea mbadala wake,”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad