Marekani: Wananchi Waandamana Kupinga Karantini



WANANCHI wa jiji la Washington DC nchini Marekani wameandamana kupinga amri ya kubaki ndani kufuatia kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Mwezi Machi, 2020,  Gavana wa Washington alitangaza hali ya dharura kama ilivyofanyika katika maeneo mengi ulimwenguni kwa kufunga migahawa, vilabu vya pombe na kupiga marufuku mikusanyiko mikubwa.


Waandamanaji wamedai kuwa haki ya watu kukusanyika kwa amani haitabadilishwa kamwe. Amri ya kubaki ndani inakiuka haki hiyo ya kikatiba.

Vizuizi hutofautiana kutoka jimbo hadi jimbo na takriban majimbo 20 yamekuwa na maandamano dhidi ya hatua hizo huku Marekani ikiripoti visa 1,010,507 na vifo 56,634 vya #COVID-19.

Kwa wiki za karibuni, Rais Donald Trump amewaunga mkono waziwazi waandamanaji. Lakini ujumbe kutoka Ikulu umekuwa ukiashiria kwamba alitaka majimbo yanayoongozwa na Democratic yapewe uhuru na kufunguliwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad