WAZIRI wa Maji,Profesa Makame Mbarawa amemuondoa kwenye nafasi yake aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Manunuzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi waMazingira jijini Tanga (Tanga UWASA) Jamal Ngereja kwa kushindwa kufanya taratibuza manunuzi ya mabomba na vifaa katika miradi saba ya maji katika wilaya nnemkoani Tanga inayotekelezwa na Mamlaka hiyo.
Pia ProfesaMbarawa amefanya maamuzi hayo katika Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingiraza Moshi,Babati na Arusha nakuahidi kuendelea kufanya mabadiliko katika mamlaka nyingine za maji zaMorogoro,Mwanza,Tabora,Shinyanga na Kahama.
ProfesaMbarawa amefikia uamuzi huo baada ya Wizara ya Maji kutoa fedha takribaniSh.Milioni 700 katika miradi saba ya maji katika wilaya zaPangani,Mkinga,Muheza na Handeni kwa ajili ya ununuzi wa mabomba tangu mweziNovemba mwaka jana lakini hakuna chochote kilichofanyika.
Pamoja na kufanya maamuzi hayo lakini pia aliwaonya wahasibu katika
mamlaka za maji nchini nao wajiandae iwapo tu watafanya uzembe katika matumizi ya fedha za miradi yamaji .“Haiwezekanitumetoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji katika mikoa ya Mbeya,Iringa naTanga kiasi hicho hicho cha fedha lakini wenzenu wamefikia asilimia 70 ya
utekelezaji lakini Tanga hakunakilichofanyika,”alisema.
Aliongeza,“ kutokana na hilo nakuambia kabisa wewe(Afisa Manunuzi) nakuondoa hapa na hilinitafanya pia kwenye mamlaka za MajiSafi na Usafi wa Mazingira za Morogoro,Mwanza,Kahama,Shinyanga na Tabora kama nilivyofanya Babati,Moshi na Arusha,”alisema.
Aidha,kwa upande wa miradi ya maji ambayo haiendi vizuri haswa ya mabwawa,ProfesaMbarawa aliahidi kuhakikisha anapeleka wataalamu kutoka wizarani kuchunguzamiradi hiyo kila kitu ilikujua kama inakwenda na thamani ya fedha zilizotumika.
“Nitahakikishakuwa ndani ya wiki kwenye miradi ya maji ambayo haiendi vizuri tunaletawataalamu kuja kuchunguza kila item(kitu)kuanzia tofali,urefu wa kibanda,kina cha mabwawa kuona kama inakwenda na valuefor money (thamani ya fedha),kutokana tumegundua kuna watu kuanzia ngazi yaHalmashauri hadi Wizarani walihusika nahujuma za miradi ya maji kwa kupandisha gharama,”alisema.
Aliongeza, “Nataka nimiambie wakandarasi nawatumishi wa Wizara ambao wamehusika nahuo mchezo mchafu wajiandae safari hii hatuna mchezo”.Katikahatua nyingine,Waziri Mbarawa amesema kuwa katika mwaka wa fedha2020/21,Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga fedha kwa ajili ya kutoa majikatika chanzo cha mto Zigi hadi katika mjiwa Horohoro wilayani Mkinga wenyeurefu wa kilometa 40.
Amesemakuwa,mradi huo utavinufaisha vijiji zaidi ya 30 vitakavyopitiwa na mradi huo nakuahidi pia kuleta wataalamu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi(DDCA) kujakuchunguza na kufanya tathminikatika bwawa la maji la Horohoro.