KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael, kwa mara nyingine tena amelazimika kufuta safari yake ya kurejea nchini Tanzania kutokana na janga Virusi vya Corona.
Kocha huyo ambaye mara baada ya Ligi Kuu Bara kusimishwa kupita Virusi vya Corona alirejea kwao Ubelgiji kwa ajili ya kufunga ndoa na mara baada ya kukamilika alitakiwa arejee wiki mbili zilizopita kabla ya kusogezwa mbele.
Akizungumza na Championi Jumatano, Eymael alisema kuwa baada ya wiki iliyopita kufuta safari hiyo ya kurejea nchini Jumamosi iliyopita kwa mara ya pili aliisogeza mbele safari hiyo.
Eymael alisema kuwa sababu ya kufuta safari hiyo ni kutokana na uwanja wa ndege wa nchini kufungwa ili kupisha janga hilo la Virusi vya Corona ambalo kila siku linaoongezeka.
“Sitaweza kuja tena kama nilivyopanga awali ni baada ya uwanja wa ndege wa huku Ubelgiji kufungwa, hivyo hakuna chochote kinachoendelea.
“Nilipanga nirejee huko Jumamosi, hivyo nimeshindwa kuja kama nilivyopanga awali, hii itakuwa mara ya pili kufuta safari yangu ya kurejea nchini Tanzania.
“Nitarejea huko baada ya shughuli kwenye uwanja wa ndege kuendelea, nilipanga kurejea mapema ili kuwahi muda wa kukaa karantini kwa siku 14 zilipangwa na Serikali ya huko lakini naona nashindwa,” alisema Eymael. Wilbert Molandi, Dar es Salaam