Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo, (Chadema), Freeman Mbowe ameikosoa taarifa ya Rais John Magufuli aliyoitoa kuhusiana na ugonjwa wa Corona kuwa haina busara.
Mbowe aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter kuwa taarifa aliyoitoa jana Ijumaa Kuu akiwa Chato mkoani Geita sio ya kistaarabu.
Amesema Rais amedai hana mpango wa kufungia wananchi sababu ya uchumi lakini ukweli ni kwamba maisha ya watu hayawezi kurudishwa.
“Maisha ya watu hayawezi kurudishwa ila uchumi utatengenezwa. Rais Magufuli, Ulimwengu unalia na kuomboleza, uchumi wa Dunia unaporomoka, uchumi wetu hauwezi ukatengamaa peke yake.Vifo vingapi vitakufanya uchukue hatua? Fanya lililo sahihi.” Aliandika Mbowe
Jana Rais John Magufuli amesema Serikali yake haina mpango wa kufungia watu ndani wala kufunga mipaka.Prez JPM speech on Corona pandemic on Good Friday at his hometown church in Chato is simply pathetic! No lockdown coz he want to save the economy & his flagship infrastructure projects. The lives of our people can not be repaired but the economy can! Lockdown or get locked out!!— Freeman Mbowe (@freemanmbowetz) April 11, 2020
Rais Magufuli amesema hayo jana Aprili 10, 2020 katika misa ya ijumaa kuu nyumbani kwao Chato, Mkoani Geita.
Rais Magufuli amesema hatua hizo ambazo hana mpango wa kuzichukua zina madhara makubwa za ndani na nje ya nchi.
Magufuli amesema kuna nchi 8 ambazo zinategema kupata huduma na bidhaa kupitia Tanzania hususani bandari ya Dar es Salaam.