Mbowe Atoka Karantini, Atinga Bungeni na “Corona”




Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amesema #CoronaVirus ni janga ambalo linapaswa kupewa uzito kama ambavyo mataifa mengine yanafanya.

Amesema japokuwa Serikali imetoa tahadhari mbalimbali, bado kuna uzembe. Ameshauri kuundwa kwa Kikosi Kazi cha Taifa ambacho kitasimamia masuala yote ya #Covid19 na kutoa wito kwa Serikali kushirikisha wadau wengine.

Ameeleza kuwa kuna umuhimu wa Kikosi hicho kushirikisha wanazuoni, madaktari, hospitali binafsi na taasisi mbalimbali ili janga hili lipewe uzito wa Kitaifa na lisibaki kwa Serikali peke yake.

 
Katika maelezo yake, Mbowe amesema tayari #CoronaVirus imeshaathiri uchumi wa nchi na alitegemea Bajeti ya Serikali ingekuja na mpango maalum na kutoa taarifa kuhusu athari hizo Bungeni, lakini mpaka sasa mipango ya Serikali ipo pale pale.


Kuhusu Uchaguzi, Mbowe amesema wamekuwa wakidai maridhiano ya nchi na #TumeHuru kwasababu wanaamini kwamba ili nchi iweze kupata maendeleo, ni lazima kuwe na viongozi wanaopatikana kwa misingi ya Demokrasia.

Amesema Kifungu no. 74 na 75 cha Katiba kinahitaji marekebisho machache na endapo upande wa Serikali utaonesha ushirikiano, maridhiano yatakuwepo na Uchaguzi utakuwa wa haki.

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haa..!! Haaa...Kulikoni.????
    Huu si uuwaji dhahiri batili.

    Huyu ni wa kujitenga..kama ni Ruzuku
    basi tumkate asilimia kadha na za deleva na kwenda Jimboni ajili asiweze
    kuwapigia chafya wana Hai kulinda UHAI
    Kulinda Uhai wao asilimia 65 mpaka 70
    ni sawa. Chonde Chonde kwa Usalama wako na wetu. Ingia machimbo. agaa kwa
    njia muwafaka.

    STAY HOME/ PROTECT NHS / SAVE LIFE

    ReplyDelete
  2. Nnavyo jua mimi Mwenye Dhamira ya kuuwa ni muuaji. Nasiyo mpaka ashike
    Silaha mkononi. and its an offence punishable by Law.

    Haa..!! Haaa...Kulikoni.????
    Huu si uuwaji dhahiri batili.

    Huyu ni wa kujitenga..kama ni Ruzuku
    basi tumkate asilimia kadha na za deleva na kwenda Jimboni ajili asiweze
    kuwapigia chafya wana Hai kulinda UHAI
    Kulinda Uhai wao asilimia 65 mpaka 70
    ni sawa. Chonde Chonde kwa Usalama wako na wetu. Ingia machimbo. agaa kwa
    njia muwafaka.

    STAY HOME/ PROTECT NHS / SAVE LIFE

    ReplyDelete
  3. STAY HOME MAANA YAKE JIKARANTINI ULIPO

    Nnavyo jua mimi Mwenye Dhamira ya kuuwa ni muuaji. Nasiyo mpaka ashike
    Silaha mkononi. and its an offence punishable by Law.

    Huu si uuwaji dhahiri batili.
    HATUCHEZI DISKO HAPA LA CHOGGY SLAY

    Huyu ni wa kujitenga..kama ni Ruzuku
    basi tumkate asilimia kadha na za deleva na kwenda Jimboni ajili asiweze
    kuwapigia chafya wana Hai kulinda UHAI
    Kulinda Uhai wao asilimia 65 mpaka 70
    ni sawa. Chonde Chonde kwa Usalama wako na wetu. Ingia machimbo. agaa kwa
    njia muwafaka.

    STAY HOME/ PROTECT NHS / SAVE LIFE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad