Mbunge Amtaja Waziri Aliyekataa Kukaa Karantini



Mbunge wa Konde Visiwani Zanzibar, kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Khatibu Said Haji, amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aingilie kati ikiwezekana kumchukulia hatua stahiki Waziri kutoka visiwani humo aliyekataa kukaa karantini, ili hali ana dalili za ugonjwa wa Virusi vya Corona.
 .

Hayo ameyabainisha Bungeni Dodoma wakati wa Mkutano wa 19, kikao cha tano cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo amemtaja jina Waziri huyo kuwa ni Salama Aboud Talib na kudai kuwa kiburi hicho anakipata wapi ili hali alikuwa anahatarisha maisha ya watu wengine.

"Kuna mchezo, mzaha na dharau juu ya maisha ya watu wa Zanzibar juu ya ugonjwa huu wa Corona, Kuna Waziri mmoja alikuwa safari ya nje aliporudi Zanzibar katika hali ya kuumwa akakataa kukaa karantini, Waziri huyu Salama Aboud Talib alienda kukaa nyumbani kwake, alipozidiwa alirudi hospitali ya Mnazi Mmoja ndani ya muda wa siku 3 aling'ang'ania" amesema Mbunge Khatibu.

Aidha Mbunge aliendelea kusema, "Alipotolewa kwa nguvu ndiyo akakubali kuwekwa karantini athari yake sasa nyumbani kwake kaambukiza watatu, hospital ya Mnazi Mmoja hatujui, je kiburi hiki kakitoa wapi?, sasa ni heri awe marehemu yeye kuliko wengine".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad