Mbwembwe za Billnass baada ya kumvisha pete Nandy



Rapa Billnass ameeeleza kuwa anataka kuheshimika kwa sababu anataka kuitwa bwana harusi mtarajiwa au shemeji, pia amewataka watu kuweka vitu vinavyoeleweka ambavyo anaweza akasoma mbele ya mkewe "Nandy".

Billnass ameeleza hilo kupitia "Tweet" mbili ambazo ameziandika kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ambazo zinasema,

"Nyie wahuni jitahidi kuweka tweet ambazo naweza kusoma mbele ya mke wangu, si  mnajua sasa hivi mimi sio muhuni mwenzenu, mambo ya pisi kali na uweka hazina nakabidhisha majukumu hivi karibuni".

Aidha kwenye Tweet ya pili ameongeza kuandika  "Jamani  tuheshimiane kidogo ukishindwa kuniita bwana harusi mtarajiwa niite hata shemeji, hivi kweli hamuogopi mume wa mtu mtarajiwa, unamuita mpwa, baharia au eti ooh mpwa unasaliti chama, hizi kauli za kihuni kwanza chama ndiyo nini CUF au Chama wa Simba"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad