Mshereheshaji wa Sherehe na shughuli mbali mbali Taji Liundi maarufu kama Master T ambaye ni mkongwe kwenye fani hii ameandika kuhusu kupungua kwa akiba ya mfuko wake kutokana na kukosa kazi za kufanya Sababu ya ugonjwa wa COVID-19 ( Corona ).
Taji Liundi ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram haya…>>>
AKIBA INAISHA
“Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi. Mimi ni Mshereheshaji.Djs wangu hawajafanya kazi Kumbi zimefungwa zote, Watengeneza cakeWapambaji wengi wanalalamika sana. Event Planners wanakosa kazi. Hadi caterers wakubwa wanalia.
”Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa. Sikujiandaa. Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili. *Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu. *Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.
“Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati. Nitamkopa nani? Nitakopa wapi?Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize? Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu..?Wewe ungefanya nini? Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!
“Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi. Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko. Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima. Tufanyeje? Tutoke turisk?Tukae bila ajira tufilisike?
“Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli. Kila siku. Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.
Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.“