Mchina aliyegoma kujikinga na Corona Ahukumiwa



MAHAKAMA ya wilaya ya mpanda mkoani katavi imemuamuru Lin Gisong (34) ambaye ni raiya wa kigeni kutoka nchini china kulipa faini ya sh 100,000 au kwenda jela miezi 6 kwa kushindwa kutekeleza sheria iliyowekwa na serikali ya kujikinga na virusi vya Corona.

Gisong alitenda kosa hilo Aprili 5 mwaka huu majira ya saa 7:30 mchana katika kata ya kasansa halmashauri ya wilaya ya mpimbwe mkoani katavi kwa kukataa kunawa mikono kwa maji tiririka.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera alisema mtuhumiwa alikuwa na mkalimani wake aliyetambulika kwa jina la James Mpepo ambaye alitekeleza agizo la kunawa mikono.

” Kwamba tulikuwa na changamoto moja ya mchina Mr Lin ambaye alitokea katika mkoa wa Rukwa akaingia katika mkoa wa Katavi kata ya kasansa mchina huyu alikuwa na mkalimani wake ambapo mkalimani alikubali kunawa mikono yeye alikataa,” alisema homera.

Homera alisema mtuhumiwa alikili kutenda kosa hilo na kudai alikuwa tayari amenawa mikono yake kule alikotoka hivyo alikubali kulipa faini ya kiasi cha sh 100,000 na sasa yuko huru na anaendelea na shunghuli zake.

“Alifunguliwa kesi namba MTO/IR/172 ya 2020 kosa kukataa amri halali ambapo alihojiwa na kuandikiwa maelezo ya onyo na askari namba F.4373D/CPL James,”alisema homera.

Aprili 17, 2020 Homera alitoa saa 48 kwa jeshi la polisi mkoani humo kuhakikisha linamfikisha mchina huyu mahakamani kwa kugoma kunawa mikono.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad