Mchina Ashikiliwa na Polisi Tanzania kwa Kukataa Kunawa Mikono, Asubiri Kupandishwa Kizimbani


Mambo yameanza kuwa siriazi bana. Jeshi la polisi mkoa wa Katavi linatarajia kumfikisha mahakamani raia mmoja wa China Lin Guosong (34) kwa kosa la kukiuka amri halali iliyowekwa na Serikali ya kunawa mikono kujikinga na corona.

Kamanda wa polisi mkoani humo Benjamini Kuzaga amesema Guosong ambaye ni Mfanyabiashara wa michezo ya bahati nasibu Sumbawanga alitenda kosa hilo April 5, 2020 katika kizuizi cha Ntibili Majimoto.

“Mtuhumiwa alikuwa anaendesha gari lenye namba za usajili T713 DRG Toyota Klluger akiwa na msaidizi wake James Mpepo (28) mkazi wa bomani    Sumbawanga, baada ya kufika eneo hilo mwenzake alishuka na kutii amri ya kunawa lakini yeye alikaidi,” amesema Kuzaga.

Kuzaga amesema Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ntibili Josephat Mgelwa alitoa taarifa kituo cha polisi Majimoto ambapo polisi walifika eneo hilo na kumkamata mtuhumiwa.

“Baada ya kumhoji hakuwa na maelezo yoyote, pia mwezake alimsihi kushuka ili anawe alikataa bila kuwa na sababu za msingi, polisi walichukua hati yake ya kusafiria Na.E09809632, na muda wowote tutamfikisha mahakamani baada ya sikukuu,”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad