Kupitia ukurasa wake wa twitter Jacob ambaye ni miongoni mwa makada machachari wa chama chake alitangaza kutogombea tena udiwani katika kata yake hatua hiyo ikihusishwa na kitendo cha wanachama wa chama hicho Zaidi ya 2,000 kumfuata nyumbani kwake kumshinikiza kugombea ubunge.
“Nimetangaza kung’atuka ktk Udiwani kata ya Ubungo Muda wa Madiwani utakapo isha,Sitogombea tena Udiwani Uchaguzi Ujao..! Miaka 10 Utumishi wangu ni Kwa Sababu Wana-Ubungo Mlinikopesha Imani. Tumekuwa wote wakati wa Shida na Raha,Mabonde na Milima, Ahsante Ubungo nimewasikia,”
Hata hivyo Boniphace anasema anajua wananchi wanampenda lakini kuna michakato ndani ya chama ndiyo inaweza kuamua yeye kuwa mgombea na endapo chama kitampa ridhaa atafanya hivyo.