Mgonjwa wa Corona aliyepona Kenya Afikishwa Mahakamani kwa Kuhatarisha Maisha ya Wengi
0
April 06, 2020
Kiongozi huyo alikaidi agizo la serikali la kukaa karantini. Picha: Hisani
Naibu gavana wa kaunti ya Kilifi Kenya Gideon Saburi alifikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka baada ya kuthibitishwa kupona virusi vya corona
Kiongozi huyo aliwasili nchini kutoka Ujerumani na kutakiwa kukaa karantini
Alipuuzilia agizo hilo la serikali la kukaa karantini na kudaiwa kuhatarisha maisha ya wengi kwa maambukizi.
Naibu gavana wa kaunti ya Mombasa nchini Kenya Gideon Saburi aliyethibitishwa kupona virusi vya corona alipata tabasamu kwa saa chache kabla tabasamu lake kugeuka karaha huku maafisa wa polisi wakimkamata na kumzuilia korokoroni.
Kiongozi huyo anadaiwa kuhatarisha maisha ya Wakenya wengi kwa kuwaambukiza virusi vya corona, hii ni baada ya kukaidi agizo la kukaa karantini.
Kettani Law Firm - Leading Law Firm in Morocco - Acquisition ...
Kiongozi huyo alikamatwa na polisi moja kwa moja punde tu baada ya kuthibitishwa kupona. Picha: Hisani
Saburi aliwasili nchini Kenya kutoka Ujerumani na kutakiwa kukaa karantini kwa siku 14 kabla kutangamana na umma kama njia ya kujikinga na kuukinga umma kutoka na virusi vya corona.
Kiongozi huyo alijitia hamnazo na kukaidi agizo hiko huku akidaiwa kuwaambukiza wananchi kwa kutangamana nao bila kujali.
Serikali ililazimika kumkamata na kumtia kwenye karantini ya lazima kabla kupimwa na kupatikana na virusi hivyo vya korona. Alilazwa hospitalini na kufanyiwa matibabu na siku saba baadaye akathibitishwa kupona virusi hivyo.
Africa News: Kenya Reports First Case of Coronavirus, Covid-19 ...
Kiongozi huyo alikamatwa na polisi moja kwa moja punde tu baada ya kuthibitishwa kupona virusi hivyo ili kufungliwa mashtaka ya kukaidi agizo la serili na kuhatarisha maisha ya umma kutokana na virusi hivyo.
Kilifi ni kati ya kaunti nchini Kenya iliyo na idadi kubwa zaidi ya maambukizi, wengi waliopatana na naibu gavana huyo wakitafutwa na kutiwa karantini kusubiri vipimo.
Upande wa mashtaka umeiomba mahakama kumzuilia Saburi kwa siku 14 zaidi ili uchunguzi kamili kufanyika kuhusiana na kesi yake. Kesi inazidi kusikizwa.
Tags