Mgunduzi wa Barakoa Arudi Kazini Baada ya Kustaafu


Mwanasayansi Peter Tsai aligundua Barakoa za N95 mwaka 1992 ambazo alizitengeneza zikiwa na uwezo wa kuzuia virusi kupenya, amerudi kazini baada ya kustaafu ili kugundua namna ya kuzisafisha na kutumika tena.

Hii imekuja baada ya uhitaji mkubwa wa barakoa duniani kote kwaaajili ya kujikinga dhidi maambukizi ya virusi vya Corona.

Peter Tsai alistaafu mwaka 2019, lakini tangu janga la Covid 19 lipate kuitikisa dunia, mchango wake umekuwa ukihitajika na amelazimika kurudi kazini.

Barakoa za N95 zinazoshauriwa kutumiwa na watumishi wa afya zina ufanisi asilimia 95 kwenye kuchuja, ‘N’ ni kifupi cha ‘Non-resistant to Oil’, huku 95 ikimaanisha ufanisi wake.

Mpaka hivi sasa duniani kote visa vya maambukizi ya Corona ni takribani milioni 3 huku vifo vikiwa vimefikia takribani laki mbili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad