Aliyekuwa Mkurugenzi Jamii Media (#JamiiForums) Maxcence Melo amekutwa na hatia katika kesi dhidi ya Jamhuri. Katika shtaka la kuzuia Polisi kufanya uchunguzi (Disemba 2016 walitakiwa kutoa taarifa za mtumiaji mmoja wa Jamii Forums), Max amehukimiwa kifungo cha mwaka mmoja Jela au faini ya shilingi milioni 3.
Kwa upande mwingine, Mike Mushi ameachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia, Hakimu Thomas Simba amesema aliungwa kwa makosa katika kesi hiyo.