Moni Alikuwa Anaomba 'Buku' Aje Kwetu" - Country



Msanii wa Bongo Fleva, mkali wa 'Trap', Country Boy amezunumzia siri ya kudumu kwa muungano wake na Moni Centrozone wanaounda kundi la 'MOCO' mpaka sasa tofauti na makundi mengine.

Akipiga stori na Friday Night Live (FNL), Counrty Boy amesema yeye na Moni wanafahamiana sana tangu zamani na wamepitia changamoto nyingi pamoja, ndiyo maana siyo rahisi kuwaona wakivunja uhusiano wao.

"Sisi tupo mamoja mpaka sasa kwa sababu tuliweka dhana moja kutokana na mahali tulikotokea, ukimuona Moni anafurahia, mimi au hata Young Lunya ni kwa sababu tumetoka katika hali moja", amesema Country Boy.

"Tumevuka pamoja kwenye maisha yale tunakula mlo mmoja pamoja, kuna kipindi Moni alikuwa anaomba hadi buku ili afike tulipo apate 'kampani' ya pamoja, kwahiyo ni kitu ambacho tumekuwa nacho pamoja", ameongeza.

Aidha Country Boy ameeleza furaha yake kufuatia albamu yake ya 'Yule Boy' kupata wasikilizaji wengi katika mitandao ya kusikiliza muziki, ambapo mpaka sasa imefikia wasikilizaji milioni 1.

Hivi sasa anatamba na wimbo wa 'Serikali Kuu' alioufanya na pamoja na Young Lunya, Moni Centrozone, Salmin Swaggz, Deddy na Zim.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad