Mpenzi au Mke Hapigwi "Mimi Nitampiga Magumi ila Kwa Kuzingatia Utaratibu Ufuatao"



Kumekuwa na mijadala kuhusu kama mwanaume anaruhusiwa kumpiga mpenzi ama mke wake. Baadhi wakisema mwanamke hapaswi kupigwa na wengine wakisema ni sahihi kupigwa.

Mimi binafsi nasema kuwa ninaweza kumpiga mke/mpenzi wangu kama itafikia hatua nitaona hakua sulihisho zaidi ya kipigo. Lakini hadi kufika huko ni lazima nipitie katika hatua hizi.

KUSUBIRI AJIREKEBISHE MWENYEWE.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa. Inafahamika wazi kuwa unapokuwa na mahusiao na mtu basi unaamini mtu huyo ni mtu mzima mwenye akili timamu lakini pia sisi binadamu si wakamilifu hivyo tunaweza kukosea wakati wowote.

Hivyo ikitokea mpenzi/mke wangu akakosea jambo Fulani kwa mara ya kwanza sitasema chochote ila nitatengeneza tu mazingira yatayofanya afahamu kuwa nimejua kuwa katenda kosa au jambo ambalo halijanifurahisha. Yeye ni binadamu huenda alipitiwa hivyo nitampa nafasi ya yeye mwenyewe kujirekebisha bila mimi kusema chochote. Kama anajitambua na pia anayapa thamani mahusiao yetu atajirekebisha na kujitahidi kutorudia kosa lile lile.

KUONGEA NAYE KUHUSU JAMBO LINALONIKWAZA.
Hatua hii itafuata kama tu kama hatua ya kwanza haitazaa matunda. Nitazugumza naye kuhusu jambo ambalo mimi linanikera. Nitahitaji kusikia utetezi wake, labda kama kuna sababu ya msingi kufanya vile ambayo labda mimi siifahamu.

Na kama atanipa sababu yenye mantiki ya yeye kufaya hivyo na nikaielewa basi, nitamuomba msamaha kwa kumfikiria vibaya.
Lakini kama mwisho wa mazungumzo akakiri kuwa kakosea basi nitamsamehe kama akinomba msamaha na hata kama pia asiponiomba msamaha, ila kwa kuwa yeye mwenyewe atakuwa amekiri kuwa kakosea; nitamuomba kwa upole na upendo mkubwa kuwa asirudie tena nitamuomba aweke ahadi kwangu hatoweza kurudia jambo hilo.

MAAMUZI YA MWISHO
Hii ni hatua ya mwisho kabisa ambayo nitaichukua baada ya hatua ya pili pia kushindwa kufanya kazi. Na maamuzi haya ni lazima yatakuwa ni moja kati ya haya; kuondoa mazingira yeye kutenda kosa, kuachana au kumpiga. Uchaguzi wa kati ya hayo mawili utategemea uzito wa kosa lenyewe na mtazamo wangu juu ya kosa lenyewe na namna linavyoathiri mahusiano yetu.

Kuondoa mazingira ya yeye kutenda kosa; hatua hii nitaifanya endapo kosa analotenda haliathiri asilimia kubwa ya mahisiano yetu. Mfano; kila tukitoka matembezi hulazimisha kufanya vitu ambavyo havikuwapo kwenye ratiba kiasi cha kupoteza muda ama pesa pasipo sababu za lazima basi nitaacha zoezi la kutoka naye matembezi. Hii itamfanya yeye asifanye hilo kosa lile lile tena na tena kwa kuwa hatakuwapo katika mazingira yatakayokuwa yananfanya yeye atende kosa hilo.

Kumpiga; hili nitalifanya kama tu kosa analofanya linaathiri pakubwa mahusiano yetu lakini linaweza kuruhusu yeye kupewa nafasi chache sana za ziada ili kujirekebisha. Kwa mfano suala la kuonyesha viashiria vya kuwa na mahusiano ya siri a mtu mwingine.

Na kipigo nitakachompiga ni kofi (sio ngumi) moja ama mawili lakini yasiyozidi matatu ambayo yatakuwa na ujazo wa kutosha kabisa ku’restore setting za ubongo wake. Na badala ya makofi hayo sitaongeza kofi linguine ama neno lolote, haijalishi yeye atafanya nini. Kwani kuongeza neno ama makofi ya ziada itafanya akasirike zaidi na kufanya ashindwe kulitambua kosa lake ama kukugeuzia kesi wewe na kosa lake akaliona si kosa kubwa ila kosa la kumpiga yeye ndilo likawa mada kuu.

NB. Mimi kumpiga yeye ni moja ya alama kubwa kabisa ya kumuonyesha bado nampenda, nathamini uwepo wake kwangu na napenda tuendelee kuwa pamoja.

Kuachana; maamuzi haya nitayachukua endapo atafanya kosa ambalo linagharimu pakubwa mahusiano yetu na pia halimpi nafasi yeye kupewa nafasi nyingine. Mfano, kubaini pasipo shaka kuwa ana mahusiano ya siri na mtu mwingine. Hatua hii inaweza kuchukuliwa hata kama kosa hilo halikupitia hatua nilizozitajwa hapo juu, linaweza kuwa ni kosa la kwanza na mahusiano/ndoa ikaisha hapo hapo.
Niliyoyaeleza hapa yanaweza yakafaya na yeye pia kwa upande wangu.

NB: USIMPIGE MPENZI/MKE/MME WAKO KIASI CHA KUMSABABISHA MAJERAHA NA KUHATARISHA USALAMA WA AFYA YAKE, NI KOSA KISHERIA.

KAMA UMEMCHOKA MTU MWAMBIE MAPEMA ILI MUACHACHANE/MTENGANE KWA AMANI KUEPUSHA MIGOGORO NA MADHARA YASIYO YA LAZIMA.
MAPENZI HAYAA FORMULA, ILA NI VEMA KUJIWEKEA MISINGI YA KUKUONGOZA.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad