Mrema Aeleza Anavyoongoza Chama kwa WhatsApp



Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema, amesema kuwa kwa sasa amekubaliana na viongozi wenzake, kufanya mazungumzo yote yanayohusu chama kupitia makundi mbalimbali ya WhatsApp waliyoyaunda ikiwa ni tahadhari ya Virusi vya Corona.



Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Aprili 3, 2020, Mrema amesema kwa sasa yeye hatoki kabisa nje mara nyingi amekuwa akibaki ndani na wajukuu zake na kutoa msisitizo kwa watu wengine pia, kama hawana sababu zozote zinazowafanya watoke nje ni bora wabaki nyumbani.

"Kwa sasa mimi sifanyi mienendo isiyo ya lazima, kama ni ofisi tumekubaliana na Katibu Mkuu kuna mambo yeye anaweza kuyafanya, Mei 5 tutakuwa na Mkutano Mkuu kwa ajili ya kumpitisha Rais Magufuli kuwa mgombea wa chama chetu, kwahiyo mawasiliano yote tunayafanya kwa njia ya makundi ya WhatsApp" amesema Mrema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad