Mrema Amuonya Mbatia 'Kuua Upinzani'


Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema, amemtaka Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia asitumike kuvimaliza vyama vingine vya upinzani, ambapo amesema itafika mahali na yeye chama chake kitakufa, ikiwa ni miezi michache baada ya Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu, kutangaza kujiunga na chama hicho Ubunge wake ukifikia mwisho.

Mrema ameyasema hayo wakati wa mahojiano, maalum na EA RadIO na EATV Digital, ambapo James Mbaria ni miongoni mwa watu ambao, alikuwa ndani ya NCCR - Mageuzi, alipelekea chama hicho kupoteza idadi ya Wabunge.

Mrema amesema kuwa "Mbatia nilikuwa naye NCCR - Mageuzi akiwa mpinzani mkubwa na akapelekea NCCR kufika hapa ilipo, akiwa mkubwa asiue vyama vingine,kama lengo lake ni kuua wenzake itafika mahali atauliwa yeye."


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad