Mrembo Hamisa Mobetto Adaiwa Kuishi Kwenye Nyumba TUPU Isiyo na Vitu vya Ndani
0
April 08, 2020
HIVI karibuni maneno yalisambaa mitandaoni kwamba mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto hana samani za ndani hivyo aache majigambo, baada ya maneno hayo kutikisa, mwenyewe ameibuka na kukanusha vikali maneno hayo.
Akizungumza na Risasi Vibes baada ya kusomewa mashtaka hayo, alijibu kuwa watu wamuache kwani hawamjui vizuri. “Watu hawajui vizuri maisha yangu, hivyo waache kunisema, siwezi kuweka kila kitu mtandaoni kama wanavyotaka wao. Wana uhakika kama ndani kwangu sina samani?” Alisema Mobeto.
Sababu ya mrembo huyo kusemwa ni baada ya Mobeto kujirekodi video kupitia mtandao mpya wa Tiktok akiwa kwenye nyumba ambayo haina kitu, ni kama ukumbi tu, hivyo watu kudai kuwa amepanga nyumba kubwa wakati hana vitu vya kuweka ndani.
Tags