Msanii Marioo Kuingia LEBO ya Harmonize...Mwenye Afungukaaa Haya


BAADA ya kuwepo kwa tetesi kuwa huwenda msanii wa Bongo Fleva, Omary Mwanga ‘Marioo’ yupo mbioni kusajiliwa kwenye Lebo ya Konde Music Worldwide au Konde Gang inayomilikiwa na Rajab Abdul ‘Harmonize’, mwenyewe amechomoa ishu hiyo.

Marioo ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, jambo hilo halipo. Marioo amesema kuwa, siyo siyo kweli kwamba ana mpango wa kusajiliwa na Konde Gang, bali kwa sasa ana mpango wa kuanzisha lebo yake mwenyewe.


“Sina mpango wa kusajiliwa Konde Gang na wala huo mpango haujawahi kuwepo, lakini binafsi natarajia kuja na lebo yangu.

“Hata hivyo, sina bifu na msanii yeyote yule hata Harmonize ni ndugu yangu sana na tunashirikiana kwenye mambo mengi,” amesema Marioo ambaye kabla ya kuhusishwa na Konde Gang pia kulikuwa na tetesi za kusajiliwa Lebo ya Wasafi.

Stori: Memorise Richard, Dar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad