Msanii wa Bongofleva Dudubaya Awagomea Tena Basata...Atangaza Kuacha Muziki



Msanii wa Bongofleva nchini Tanzania,Tumaini Godfrey maarufu Dudu Baya amegomea wito wa Baraza la Sanaa Tanzania(Basata).

Hii ni mara ya pili kwa Dudu Baya kuvutana na baraza hilo,ambapo Januari 7,mwaka huu walipomuita kuhusiana na kuweka video katika mitandao ya kijamii zikiwa na maneno yasiyokuwa na staha, aligoma kwenda hadi kufikia hatua ya kufungiwa kutojihusisha na sanaa lakini baadaye Februari, 2020 Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alitangaza kumsamehe.

Baada ya msamaha huo DuduBaya aliahidi kujirekebisha.

Sambamba na kugomea wito huo pia DuduBaya ametangaza kujifuta rasmi kuwa msanii kwa kile alichoeleza kutoridhishwa na figisufigisu zinazoendelea kwenye tasnia ya sanaa.

Amesema mbali na hilo pia Basata haichukulii hatua malalamiko mbalimbali ambayo wamekuwa akiyawasilisha kuhusu sanaa.

Hatua hiyo ya DuduBaya imekuja baada ya Aprili 14, 2020 Basata kumwandikia barua ya wito ambayo ilisainiwa na katibu wa baraza hilo, Godfrey Mngereza.

Barua hiyo ilimtaka kufika leo Jumanne Aprili 14 katika ofisi zao zilizopo Ilala Sharif Shamba, saa 3:00 asubuhi.

"Wito huu umetokana na wewe kuonekana katika mitandao ya kijamii ukitumia lugha zisizo za staha ukiwa kama msanii unayetakiwa kuzingatia maadili mema katika jamii

"Ikumbukwe kuwa usipofika taratibu nyingine zitafuata kwa mujibu wa sheria ya baraza na kanuni zake bila ya kukupa taarifa nyingine, "ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
Mwananchi ilifika ofisi za Basata saa 3:00 na kuelezwa kuwa msanii huyo bado hajafika na Hadi inaondoka eneo hilo saa tano asubuhi alikuwa hajafika jambo lililosababisha kumtafuta kujua sababu.
Akizungumza kwa njia ya simu, DuduBaya amesema ni kweli hajaenda kama alivyotakiwa na kueleza sababu kuwa wamemfungia akaunti ya Instagram.
Kutokana na hilo alimpigia Mngereza kumueleza namna alivyochukizwa kufungiwa hivyo hata ofisini kwao hatakwenda tena.

“Mimi kuanzia sasa siyo msanii, nimejitoa rasmi katika sanaa, waambieni na nimeshawaambia”amesema DuduBaya.
Mngereza amesema kuwa wanaendelea na hatua nyingine na kufungiwa kwa akaunti ya instagram ya msanii huyo haiwahusu.
“Kujifuta usanii hakutuzuii kumchukulia hatua zaidi, hilo la kujitoa katika sanaa amelisema yeye na sisi tunafanya kazi yetu kwa mujibu wa sheria,”amesema Mngereza.


Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dudu Baya, Nakusihi, usichukulie hasira

    Ulichozuungumza NDIYO UKELIHAISI.

    NIJUU YA WIZARA AMBAO WAMEKWISHA LIONA HILO NA WANALISHUGHULIKIA KWA WASANI WOTE TOKA WALIO SHINDA MIAKA YA NYUMA 2013 - 2019.

    Hawa MATAPELI WANAOVAA BRAZILIANN HAIR NA MAGARI KUBADILISHA MADIWANI MKUBWA NA GENGE LAKE KUWADHULUMU HAWA VIPAJI CHIPUKIZI.

    AWAMU HII HAWATOFUMBIWA MACHO.

    MWAKYEMBE NA SHONZA NI WAELEWA NA NI
    WAADILIFU.

    MACHUNGU YAKO NA JAZBA TUMEKUELEWA KAK.

    TAFUTA WAKATI MUAFAKA UKIPENDA.

    ReplyDelete
  2. Dudu Baya, Nakusihi, usichukulie hasira

    Ulichozuungumza NDIYO UKELIHAISI.

    NIJUU YA WIZARA AMBAO WAMEKWISHA LIONA HILO NA WANALISHUGHULIKIA KWA WASANI WOTE TOKA WALIO SHINDA MIAKA YA NYUMA 2013 - 2019.

    Hawa MATAPELI WANAOVAA BRAZILIANN HAIR NA MAGARI KUBADILISHA MADIWANI MKUBWA NA GENGE LAKE KUWADHULUMU HAWA VIPAJI CHIPUKIZI.

    AWAMU HII HAWATOFUMBIWA MACHO.

    MWAKYEMBE NA SHONZA NI WAELEWA NA NI
    WAADILIFU.

    MACHUNGU YAKO NA JAZBA TUMEKUELEWA KAK.

    TAFUTA WAKATI MUAFAKA UKIPENDA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad