Mbunge wa Iringa mjini ( Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amesema maambuki ya ugonjwa wa Corona yanaongezeka ni lazima watu wafungiwe ndani ili kuzuia maambukizi.
” Pona yetu ni kujikinga tu! Complete lockdown haiepukiki. Mipaka ya yote ya nchi ifungwe,” ameandika Msigwa katika ukurasa wake wa twitter.
Alisema kila mwanachama afungiwe ndani kwa miezi mitatu kwa lazima.
“Serikali ya wanyonge isaidie wanyonge chakula ivunje kibubu chote cha taifa,’ amesema Mchungaji Msigwa.
Hakuna namna. Maambukizi na vifo vinaongezeka. Pona yetu ni kujikinga tu! Complete lockdown haiepukiki. Mipaka yote ya nchi ifungwe. Kila mwananchi afungiwe ndani angalau kwa miezi mitatu kwa lazima. Serikali ya Wanyonge isaidie wanyonge chakula. Ivunje kibubu chote cha taifa..— peter msigwa (@MsigwaPeter) April 11, 2020
Mimi nilimwambia M/Kiti akae siku 60
ReplyDeleteNadhani ameogoea RUZUKU Msije mkatia Ndani katika hiki kipindi cha LALA SALAMA.
UNLESS UMUAHIDI KAMA MTAMTUMIA TIGO PESA. UNAWEZA KUMUAHIDI HIVYO ILI
ASALIMIKE NA ATUSALIMISHE..!! Selasini