Mtoto wa Mama Rwakatare Anena Majibu ya Wataalam Kifo Cha Mama yake



Mtoto wa kiume wa Mchungaji na Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto, Muta Rwakatare, amesema kuwa mpaka sasa wanasubiri majibu kutoka kwa wataalam ili kujua ni kipi hasa kilichopelekea kifo cha mama yao licha ya kuwa alikuwa akisumbuliwa na presha.

Hayo ameyabainisha leo Aprili 20, 2020, wakati wa mazungumzo maalum na EATV, ambapo amesema kuwa kwa sasa wanafamilia watakaa na kujua mazishi yatafanyika kwa namna gani, huku wakishirikiana kwa pamoja na Serikali.

"Amefariki leo na alikuwa yupo Hospitali, alikuwa na matatizo kidogo ya presha, kwahiyo mpaka sasa hivi tunasubiri majibu kutoka kwa wataalam tujue amepatwa na tatizo gani haswa" ameeleza Mtoto wa Marehemu Mama Rwakatare.               

Mheshimiwa Askofu Mama Getrude Rwakatare, amefariki Dunia Alfajiri ya leo, katika Hosptali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad