Muhumbili Yafunga Mashine Kusafishia Figo Amana


Hospitali ya Taifa Muhimbili imefunga mashine tatu zakusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo na inatarajia kufunga mashine moja ya kusaidia kupumua (ventilator) Hospitali ya Rufaaa Amana kwa wagonjwa wa Corona.

Tayari wagonjwa wanaohitaji huduma ya kusafishwa damu wameanza kuhudumiwa na wafanyakazi wa MNH waliopo Hospitali ya Amana tangu Aprili 24, 2020 ambapo dawa na vitenndea kazi vya kutoa huduma ya kusafisha figo kwa sasa vinagharamiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mashine hizo tatu zilizofungwa na hospitali ya Muhimbili zenye gharama ya Tsh milioni 210 na inatarajia kufunga mashine moja ya kusaidia mgonjwa kupumua (ventilator) yenye thamani ya TSh. Mil 56 katika Hospitali ya Rufaa Amana ili kuhudumia wagonjwa wenye maambukizi ya virusi Corona

MNH pia imefunga mtambo wa kuchuja maji (Portable RO) wenye thamani ya Tsh. Mil 28 na mtandao wenye miundombinu ya kusafirisha maji ili kuwezesha mashine hizo kufanya kazi ya kusafisha damu uliogharimu Tsh. Mil 12.

Aidha MNH inatarajia kupokea madaktari na wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana kuanzia April 28, 2020 ili kujengewa uwezo kwenye Kitengo cha Kusafisha Damu pamoja na vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICUs) aina tano tofauti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad