Muna Love Kufanya Upasuaji Kupunguza Tumbo na Pua..


WATU wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi juu ya aina ya ulokole wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Rose Alphonce ‘Muna’.  Hii ni kutokana na mavazi anayovaa na jinsi anavyojiweka kwa maana ya ‘life style’ kiasi cha watu kutilia shaka ulokole wake.

Katikati ya mkanganyiko huu, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limefanya mahojiano maalum (exclusive) na Muna kuhusiana na ulokole wake kutiliwa shaka. Muna anasema kuwa, baadhi ya watu wanachukulia ulokole ni kuwa rafu na kuonekana tofauti, jambo ambalo si kweli. Zaidi ya hilo, pia Muna amefunguka juu ya mpango wake wa kufanya upasuaji kupunguza tumbo na kurekebisha pua yake. Dondoka naye;

IJUMAA WIKIENDA: Mambo vipi Muna! Umekuwa kimya, vipi ukimya wako una kitu gani?

MUNA: Niliamua tu kufanya mambo yangu na niliona ni bora kufanya vitu kimyakimya maana hata ukifanya jema, bado kuna watu hawataliona hilo jema, zaidi sana watakutafutia ubaya tu.

IJUMAA WIKIENDA: Vipi kuhusu ishu ya kufunga ndoa kwa sababu ilizagaa tu mitandaoni kwamba umebadili dini na kuolewa, hii ishu ilikuwa imekaaje?

MUNA: Hiyo ishu ikae hivyo hivyo, lakini watu wajue tu kwamba siwezi kubadili dini. Ipo siku nitaweka wazi ni kitu gani kilitokea. Kwa upande wa ndoa, watu wazidi kuniombea maana niko kwenye mikakati hiyo.

IJUMAA WIKIENDA: Lakini kuna maneno mengi yanasemwa kutokana na uvaaji wako, kwenda kwenye kumbi za starehe na wewe ni mlokole, unalizungumziaje hilo?

MUNA: Watu wanashindwa tu kuelewa, labda wanataka ukiwa mlokole uwe mchafu na hata usiende kuhudhuria vitu vya watu wako wa karibu! Kwa mfano nilikwenda kwenye uzinduzi wa Albam ya Harmonize kwa sababu yule ni kama familia. Pia siwezi kuacha kupendeza na kuvaa vizuri kwa kuogopa watu. Mungu anataka tuwe wasafi wa moyo na mwili pia.

IJUMAA WIKIENDA: Sasa hivi mara nyingi ukiangalia ukurasa wako wa Instagram, baadhi ya watu wanakuita jina la mwanamuziki marehemu Michael Jackson, ni kwa nini?

MUNA: Hata mimi nimelipokea hilo jina kwa mikono miwili. Hata hivyo, nina mpango wa upasuaji au marekebisho kwenye mwili wangu kama kupunguza tumbo na kubadilisha pua.

IJUMAA WIKIENDA: Kwa nini unasema jina hilo la Michael Jackson umelipokea kwa mikono miwili?

MUNA: Nimelipokea kabisa kwani huoni hata ngozi yangu imebadilika kabisa? (amekuwa mweupe mno tofauti na zamani).

IJUMAA WIKIENDA: Vipi kuhusu ile ishu ya mtoto uliyedaiwa kuzaa na kumtelekeza Moshi kwa kuwa hukutaka kumuweka wazi?

MUNA: Kwanza ijulikane wazi kuwa mimi nina watoto wengi ninaowalea, sasa iweje mtoto wangu kabisa nisiwe na uchungu naye? Nitakuwa ni mwanamke wa aina gani?

IJUMAA WIKIENDA: Hivi karibuni ulionekana kuwa na mawasiliano na mwanaume shoga wa Nigeria, watu wakakutolea maneno machafu na kuona kama siyo sahihi kwa mtu wa Mungu kufanya hivyo. Je, unalizungumziaje hili?

MUNA: Hivi jamani Mungu anawahitaji watu wema au wenye dhambi? Siwezi kuwachukia watu wa aina hiyo hata kidogo kwa sababu inawezekana wanaowasema vibaya wanaweza wasipokelewe kwa Mungu, lakini wao wakitubu dhambi, wakienda kwa Mungu, watapokelewa.

IJUMAA WIKIENDA: Kila wakati unaonekana ni mtu wa kufanya ‘make-up’ sana, kwa nini?

MUNA: Kwa nini nikae bila kufanya make-up? Yaani huyo anayenifanyia make-up akiwa hayupo mjini nitateseka sana. Mimi bila kuweka sura yangu vizuri nahisi sijakamilika kwa kweli.

IJUMAA WIKIENDA: Vipi kuhusu Wema Sepetu ambaye alikuwa rafiki yako mkubwa, mnaongea kama kawaida?

MUNA: Watu wanashindwa kuelewa, mimi na Wema hatuna tatizo lolote na hata walivyosema nimeiba kufuli yake, hawajui tu nilivyoumia, lakini kwa vile Mungu ni mwema, atawaonesha.

IJUMAA WIKIENDA: Vipi kuhusu uhusiano wako na mwimba Injili, Emmanuel Mbasha maana haieleweki mna uhusiano gani au kuna nini kati yenu?

MUNA: Mbasha ni mshkaji wangu sana na huwa tunataniana. Hakuna kinachoendelea kati yetu.

IJUMAA WIKIENDA: Siku za nyuma kulikuwa na kutokuelewana kati yako na familia yako, vipi mmeshamaliza tofauti zenu?

MUNA: Sipendi kuzungumzia familia yangu kwenye vyombo vya habari ndiyo maana nilikuwa siwezi kueleza chochote hata kipindi kile.

IJUMAA WIKIENDA: Wiki kadhaa zilizopita ulisema umekwama China kwa sababu ya Virusi vya Corona, imekuwaje ukafanikiwa kurudi?

MUNA: Baada ya kuona virusi vinasambaa, nilirejea kupitia Nairobi (Kenya) ndipo nikapata upenyo wa kurudi Tanzania

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad