Mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ualbino afariki kwa ajali ya gari


Mwanza. Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner  Foundation Europe  (JTFE), inayojishughulisha na masuala ya watu wenye ualbino, Josephat Torner amefariki dunia kwa kugongwa na gari jijini Mwanza.

Torner ambaye pia ni mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ualbino nchini Tanzania, amepoteza maisha saa 2:00 usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2020 baada ya kugongwa na Hiace wakati akivuka barabara mbele kidogo ya daraja la  la watembea kwa miguu Furahisha.

Mwanaharakati huyo amepoteza maisha wakati akipelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Sekoutoure.

Taasisi yake imekuwa ikiwafadhili wanafunzi wenye ualbino kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu ndani na nje ya nchi.

Polisi mkoani Mwanza wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha kifo chake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad