Mwigulu Nchemba "Serikali isitangaze Wagonjwa Wapya wa Covid19"
1
April 15, 2020
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ameishauri Serikali kutangaza idadi ya watu wanaopona au kufariki pekee na kuacha kutangaza idadi ya wagonjwa wapya wa ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19) unaoambukizwa na kirusi cha Corona wanaogundulika kila siku hapa nchini kama ambavyo inafanya sasa
“Mimi naona zibaki taarifa za aina tatu tu, (uwepo wa ugonjwa, waliopona na waliofariki). Hivi tunavyotoa taarifa ni kama nchi zinashindana, sijui kwanini wengine wanatamani takwimu ziwe nyingi na kuwe na wagonjwa wengi. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa jambo la "kipumbavu" likisemwa kizungu linaonekana la maana, labda kwa sababu Corona ilianzia majuu basi mnaona sifa" Alieleza Nchemba
Tuandikie hapa maoni yako juu ya ushauri huu wa Waziri wa Zamani wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Ndani
Tags
Ni mtazamo wake na sio mbaya,lkn km Mimi naona Watangaze idadi ya wagonjwa,ikibidi watangazwe hata majina yao kabisa tuyajue ili nasi tujue km tuliwai kukutana nao ili tujue namna ya kujitenga na kukaa karantini,huu ni ugonjwa hatari na c rahisi kwa mgonjwa kuwajua wote aliokutana nao
ReplyDelete