Mzee wa miaka 58 adaiwa kubakwa na vijana wawili


Serengeti. Polisi wilayani hapa mkoa wa Mara wamemkamata mtuhumiwa mmoja kati ya wawili wanaodaiwa kumbaka mama mmoja mwenye umri wa miaka 58, mkazi wa Miseke

ambaye amelazwa hospitali Teule ya Nyerere kwa ajili ya matibabu.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Aprili 6 usiku katika kitongoji cha Senta wakati mama huyo (jina limehifadhiwa), mkazi wa kitongoji cha Majengo akitoka kutafuta tumbaku na mboga na inadaiwa watuhumiwa walimfuatilia kwa nyuma na kumkaba na kumfanyia ukatili huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah aliliambia Mwananchi kwa njia ya simu jana kuwa mtuhumiwa Kumari Mongita (23) mkazi wa kijiji cha Miseke amekamatwa na mmoja wanaendelea kumtafuta kwa kuwa alikimbia.

“Watuhumiwa walitajwa na mama huyo aliyefanyiwa ukatili na vijana hao, huyo mmoja kwa ushirikiano na wananchi tunaamini atakamatwa ili wafikishwe mahakamani baada ya taratibu kukamilika,” alisema .

Mganga mkuu wa hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba alidai mama huyo ana maumivu kifuani na sehemu nyingine za mwili.


“Anadai baada ya kumwangusha walimvua nguo na mmoja akambana kifua, mwingine alimwingilia wakifanya kwa zamu kisha wakamtupa kwenye kajito,” alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad