Ndege ya Urusi Yaelekea Marekani Na Vifaa vya Kukabiliana Na Virusi Vya Corona




Wizara ya afya nchini Urusi imesema leo kuwa ndege ya nchi hiyo iliyobeba vifaa vya tiba imeondoka nchini humo kuelekea Marekani, huku ikulu ya Kremlini ikitanua ushawishi wake wakati huu wa janga la virusi vya corona.

Video iliyotolewa na wizara hiyo, ilionyesha ndege hiyo ya mizigo iliyobeba masanduku ikijiandaa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Moscow mapema leo. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP, wizara hiyo ilikataa kutoa habari zaidi kuhusu hatua hiyo inayokuja baada ya rais wa Urusi Vladmir Putin kuzungumza na mwenzake wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu. 

Awali Urusi ilituma vifaa vya matibabu na watalaamu wa virusi vya corona katika taifa la Italia lililoathirika pakubwa kutokana na virusi hivyo kama sehemu ya juhudi zake za kibinadamu ambazo wachambuzi wanasema zimebeba ushawishi mkubwa wa kijiografia na kisiasa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad