New York Yarekodi Wagonjwa wa Corona Wengi zaidi Duniani
0
April 10, 2020
New York state sasa ina visa vingi vya virusi vya corona zaidi ya taifa lolote duniani , kulingana na takwimu mpya.
Serikali imethibitisha kwamba idadi ya visa vya ugonjwa huo imeongezeka kutoka 10,000 siku ya Alhamisi hadi 159, 937 na kuiweka mbele ya Uhispania ilio na visa 153,000 na Itali ilio na visa 143,000.
China ambapo virusi hivyo vilianza mwaka uliopita iliripoti visa 82,000. Marekani yote imerekodi visa 462,000 na takriban vifo 16,500.
Huku Jimbo la New York likiongoza ulimwengu katika visa vya maambukizi , takriban watu 7000 wamefariki katika mji huo , ikiwa nyuma ya Uhispania ilio na vifo 15,500 na Itali ilio na 18,000 ikiwa ni mara mbili ya vifo vya China 3,300.
Picha zimeonekana za watu waliovalia magwanda ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona wakiwazika watu walioifariki katika kaburi kubwa la pamoja mjini New York.
Picha zilizochukuliwa na kamera za juu zilionyesha wafanyakazi wakitumia ngazi kuingia katika kaburi hilo kubwa ambapo majeneza hayo yalikuwa yamewekwa.
Picha hizo zilichukuliwa katika eneo la Hart Island kando ya mji wa Bronx , ambao umekuwa ukitumika kwa zaidi ya miaka 150 na maafisa wa baraza la mji kama eneo la makaburi ya pamoja kwa wale wasio na familia na wasioweza kumudu mazishi.
Operesheni za mazishi katika eneo hilo zimeongezeka kutokana na mlipuko wa virusi kutoka siku moja kwa wiki hadi siku tano kwa juma, kulingana na Idara magereza.
Wafungwa kutoka kisiwa cha Rikers ndio ambao wamekuwa wakifanyakazi hiyo, lakini ongezeko la kazi limefanya kazi hiyo kuchukuliwa na wanakandarasi.
Meya wa mji wa New York Bill De Blasio amesema mapema wiki hii kwamba maziko ya umma ya mji huo huenda yakatumika wakati wa mlipuko huu.
Dkt Anthony Fauci, mwanachama wa jopo la Ikulu ya Whitehouse kuhusu virusi vya corona , aliambia NBC , kipindi cha leo kwamba idadi ya mwisho ya Wamarekani ambao watafariki kutokana na virusi vya corona huenda ikafikia 60,000.
Mwisho wa mwezi Machi Dkt Fauci alikadiria kwamba kati ya watu 100,000 na 200,000.
Utabiri huo wa 60,000 ulitarajiwa kufikia idadi ya vifo vyote vinavyosababishwa na Flu nchini humo kati ya Oktoba 2019 hadi Machi 2020 kulingana na data ya serikali.
Lakini makamu wa rais Mike Pence alisisitiza siku ya Alhamisi kwamba maambukizi ya Covid -19 ni mara tatu yale ya Flu.
Picha zilizochukuliwa kutoka juu zilionyesha miili ikizikwa katika kaburi moja kubwa la pamoja katika kisiwa cha Hart mjini New YorkHaki miliki ya pichaREUTERS
Ikulu ya Whitehouse ilikuwa imesema kwamba huenda Wamarekani milioni 2.2 wakafariki kutokana na virusi vya corona iwapo hatua hazitachukuliwa.
Agizo la kusalia nyumbani wakati huohuo limefunga bishara zisizo muhimu katika majimbo 42 huku likipunguza kasi ya uchumi wa taifa hilo.
Data mpya siku ya Alhamisi ilionyesha ukosefu wa ajira uliongezeka hadi milioni 6 kwa wiki ya pili mfululizo , ikiongeza idadi ya Wamarekani ambao hawako kazini katika kipindi cha wiki tatu zilizopita kufikia milioni 16.8.
Wakati huohuo Chicago imeweka amri ya kutouzwa kwa pombe kuanzia saa tatu siku ya Alhamisi ili kuzuia ukiukaji wa marufuku ya kupiga marufuku mikutano ya watu wengi.
Tags