Niyonzima Atupa Kombora Simba



KIUNGO mchezeshaji mkongwe fundi, Haruna Niyonzima, amesema kuwa kwa sasa ni bora akastaafi a maisha yake ya soka Yanga na siyo kurudi tena Simba.

 

Niyonzima alirejea kuichezea Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea AS Kigali ya nyumbani kwao Rwanda.

 

Kumbuka kabla ya hapo alikuwa Simba aliyoitumikia kwa misimu miwili.Kiungo huyo kutua kwake Yanga kumeimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo na kurudisha matumaini ya kufanya vema.


Mwandishi wa Spoti Xtra, Wilbert Molandi akiongea na Niyonzima.

Akizungumza na Spoti Xtra, Niyonzima alisema kuwa amezichezea klabu zote mbili kubwa na kongwe hapa nchini, lakini kwake alifurahia na anaendelea kufurahia maisha yake akiwa Yanga.

 

Niyonzima alisema ataendelea kuipambania timu hiyo kwa kipindi chote atakachokuwepo Yanga na kati ya vitu ambavyo amevipanga ni kuhakikisha anarejesha heshima ya timu hiyo ikiwemo kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo ligi kuu.

 

Aliongeza kuwa kikubwa viongozi wa timu hiyo chini ya wadhamini wao, Kampuni ya GSM kuhakikisha wanafanyia kazi ripoti ya usajili katika kuelekea msimu ujao kwa lengo la kutengeneza kikosi imara kitakacholeta ushindani.

 

“Kwa sasa nisingependa kuizungumzia timu ambayo nimetoka kuichezea kwani nipo kwenye timu yangu ya zamani ya Yanga niliyowahi kuichezea kwa furaha na amani kubwa.

 

“Kiukweli nilikuwa na furaha kubwa nikiwa Yanga kabla ya kwenda Simba, hivyo kwa sasa sifi kirii kabisa mimi kurudi tena huko, akili na nguvu zangu nimepanga kuzitumia nikiwa hapa, nafahamu mashabiki wana hamu kubwa ya ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu miwili mfululizo.

 

“Hivyo mashabiki wa Yanga waondoe hofu, mengi nimepanga kuyafanya nikiwa hapa, ninaamini bado wana furaha ya kuwafunga Simba bao 1-0 huku tukipata sare ya mabao 2-2,” alisema Niyonzima.

Stori na WILBERT MOLANDI, Dar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad