Papa afanya maombi ya njia ya msalaba bila ya watu


Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis katika jioni ya siku ya Ijumaa kuu jana amekumbusha juu ya njia ya mateso ya Yesu Kristo na kufanya maombi.

Kutokana na janga la virusi vya Corona sherehe hizo hazikufanyika katika njia maalum mjini Rome, badala yake katika eneo ambalo halikuwa na watu la uwanja wa mtakatifu Petro.

Maelezo kwa ajili ya vituo 14 vya njia ya msalaba vimetokana na wafanyakazi na wafungwa wa jela ya Due Palazzi mjini Padua.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 83 alifuatilia maombi hayo kutoka katika dirisha la kanisa la mtakatifu Petro.

Kutokana na virusi vya COVID-19 kiongozi huyo wa kanisa Katoliki atajitokeza kwa kiasi kidogo katika sherehe hizi za Pasaka. Televisheni zitatangaza moja kwa moja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad