Mchungaji James Ng’ang’a anayefahamika sana humu nchini kutokana na misimamo yake mikali, sasa ameitaka serikali kumpa ruhusa ya kuponya watu walioathirika na virusi vya Corona.
Pastor Ng’ang’a tena!,Serikali haijaweka mipango mahususi
Kwa sasa Kenya imethibitisha visa 59 vya watu walio na corona huku Nairobi ikiwa katika kipaumbele cha watu waliona corona.
Kupitia video iliyo katika mtandao wa kijamii na kuenea sana Ng’ang’a amesihi serikali kumruhusu kuponya wagonjwa,20, walio na kirusi cha Corona.
Kwa sasa ng’ang’a yuko na zaidi ya miaka hamsini na tano, na anaamini kuwa anaweza kuponya watu walio na corona kupitia gitaa yake.
Kulingana na mhubiri huyo na wenzake wana mamlaka na nguvu za kuponya wagonjwa hao na kuteseka kwa wanadamu kufika mwisho.
Ng’ang’a alisema anataka tu kupatiwa ruhusa na yale mengine yote yatakuwa sawa aliomba serikali kumpa wagonjwa 20, na kisha wawe peke yao katika chumba kwa muda na asiweze kusumbuliwa na watu kutoka nje.
‘Mniombe msamaha!’ Pator Ng’ang’a aambia shirika la reli kuhusu mzozo wa shambaAlizungumza akitumia gitaa yake anaweza kumsifu Mungu na hata kuponya walio wagonjwa, alisistiza anahitaji tu gitaa yake na nyimbo motomoto za kumsifu Mungu.
Alisema kuwa akipewa ruhusa atatumia gitaa yake na wagonjwa hao watapona, na wala hatotumia glavu wala barakoa akiwa na wao.
“If the government just gave the opportunity and brought me those patients who suffer from this virus, I would try God because he told us to try him.” Alisema Ng’ang’a.
Kuna wakati mhubiri uyo alionekana akimponya msanii wa nyimbo za injili Rose Muhando alipokuwa anasumbuliwa na ugonjwa.
Aliwauliza wananchi wasiwe na wasiwasi kwa ajili ya kirusi hicho kwa maana wasiwasi utawafanya wachanganyikiwe katika mwili wa kiroho