PAUL Makonda "Kuanzia Jumatatu Kila mtu Lazima Avae Mask na Biashara Zone Zifanyike kwa 'take awa'



Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ameagiza kuwa mtu yeyote anayeenda katika eneo lolote la manunuzi lazima awe amevaa Barakoa (mask)

Amesema haijalishi ila lazima watu wavae Barakoa “Ununue, ukate kanga, ukate leso na utafute rubber bands. Lazima uwe umevaa Barakoa”

Aidha, ameagiza kuwa kuanzia Jumatatu biashara zote zifanyike kwa mfumo wa ‘take away’ yaani ufike sehemu ya kununua bidhaa, nunua na ondoka

Pia, amewataka watu kuhakikisha wanakaa umbali wa mita 2 kila wakiwa eneo la msongamano wa watu huku akiwataka wenye masoko kutafuta mfumo mbadala na mzuri wa kusimama sokoni
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad