KAMA ulikuwa unategemea itafika siku utaona kapo ya wasanii, Rotimi na Vanessa ikivunjika basi fahamu ya kuwa wapenzi hao wameapa kutoachana.
Kauli hiyo ilitolewa na Rotimi mara baada ya kutokea katika kipande cha video ambayo Vanessa aliiweka katika ukurasa wake wa Instagram akijibu swali la kwa nini yupo kimya na hafanyi kazi ya muziki kwa sasa, huku sababu kubwa ikitajwa ni kutekwa kimapenzi.
Vanessa wakati anatoa utetezi wake kuwa siyo mapenzi yanayofanya akae kimya bali ameamua kujipa muda wa kupumzika, Rotimi akaibuka na kusema na ‘hatuachani’, kauli ambayo iliungwa mkono na Vanessa kwa kusema kuwa kwa sasa ameyapata mapenzi na anafurahia maisha.
“Ninaishi maisha mazuri na ninaenjoy sana, nimeyapata mapenzi mazuri nina furaha, kwa hiyo kwa sasa nimeamua kupumzika muziki na kujipa muda na mpenzi wangu kufurahia maisha, muda wa kufanya kazi ukifika nitarudi na mtaona nikifanya hivyo,” alisema Vanessa.