Polisi Arusha: Alberto Msando anashikiliwa kwa uchochezi dhidi ya serikali kuhusiana na corona




Jeshi la polisi mkoani arusha limefunguka sababu ya kumkamata na kumshikilia Wakili Alberto Msando na kusema kuwa amekamatwa kwa kosa la kutoa taarifa za  uchochezi dhidi ya serikali kuhusiana na ugonjwa wa corona.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha Koka Moita amesema kuwa kupitia clip ya video Msando alionekana akitoa taarifa ya uwepo wa hali mbaya ya corona kwa mkoa wa Arusha ikiwa yeye hana mamlaka ya kutoa taarifa hizo.


"Jana april 29 alikamatwa wakili Albarto Msando kwa kutoa taarifa za uchochezi kwa serikali kuhusiana na ugonjwa wa corona wakati hana mamlaka ya kutoa taarifa za corona kama ilivyotangazwa kuwa watoaji wa taarifa ni waziri mkuu, waziri wa afya na mganga mkuu wa serikali hili ni tangazo muhimu na kila mwananchi anatakiwa aliheshimu"


Jeshi la polisi limedai kuwa kauli hiyo imeleta mshtuko kwa wananchi waliokuwa wanasikiliza lakini serikali imetoa maelekezo kwa watoaji wa taarifa za ugonjwa huo.

Kwenye video hiyo Msando alisikika akisema "Ukweli ni kwamba na niseme bira kuficha hali ni mbaya Arusha na ndugu waandishi ifike mahali muweke miguu chini na mseme ukweli ili wananchi, serikali na kila anayehusuka ajue tupo kwenye hali mbaya ambapo kila mtu anatakiwa kuchukua hatua mkirudi nyuma tutazikana"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad