Pual Makonda "Hospitali 25 zatengwa Kwa Ajili ya Corona Dar es Salaam"



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema Serikali katika mkoa huo imetenga hospitali 25 kwa ajili ya wagonjwa ambao watajihisi wana dalili za ugonjwa wa Covid-19.

Amesema katika hospitali hizo zipo za umma na za watu binafsi, lengo ni kusaidia wananchi ambao hisia zao zinawapeleka kwenye corona, ili kuwalinda wananchi na watoa huduma kwani bila kufanya hivyo kutakuwa na mrorongo wa watu wengi wanaotakiwa kwenda karantini.

“Nimeona tuje na mbinu mbadala ya kutenga Hospitali 25 katika Mkoa wa DSM ambazo zitatumika kwa mwenye dalili ya homa kali na mafua makali hasa ambaye anahisi atakuwa na corona, Ilala tunazo 8, Temeke 4, Kinondoni 6, Ubungo 4 na Kigamboni tunazo 3,” amesema Makonda
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad