Putin akiri kuwa hali yazidi kuwa mbaya nchini Urusi



Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa hali ya Corona nchini humo inaelekea kubaya.

Putin, ambaye alifanya tathmini juu ya coronavirus katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika kwa njia ya video, amesema kwamba hali katika nchi yake inazidi kuwa mbaya, lakini hatua walizochukuakuudhibiti ugonjwa huo zinandelea kufanya kazi.

"Tunaona kuwa hali inabadilika kila siku na kwa bahati mbaya inazidi kuwa mbaya. Idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka, haswa idadi ya wale walio na hali mbaya inazidi" alisema.

Akisisitiza kwamba mahitaji ya taasisi zote za afya yanapaswa kutafikiwa, Putin amesema kuwa vifaa vya kinga na vifaa vya matibabu vimeamriwa kuelekezwa kwa mikoa yote yenye uhitaji.

Putin amebaini kuwa, ikiwezekana, vifaa vya jeshi pia vinaweza kutumiwa kupambana na janga hilo.

Huko Urusi, ambapo watu 148 wamekufa kutokana na  Kovid-19, idadi ya kesi za maambukizi imetangazwa kuwa18,328.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad