Qatar, Saudi Arabia zagombania uenyeji wa michezo ya olimpiki ya Asia 2030



Mataifa jirani yanayohaimiana Qatar na Saudi Arabia yatapambana kuwania uenyeji wa michezo ya olimpiki ya bara la Asia, baada ya Baraza la Olimpiki la Asia, OCA, kutangaza kupokea maombi kutoka Doha na Riyadh leo.

Rais wa Baraza hilo Sheikh Ahmad Al-Fahad Al-Sabah, amesema katika taarifa kuwa baraza limepokea maombi mawili mazito kwa ajili ya uenyeji wa michezo ya mwaka 2030.

Saudi Arabia, pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri, zilivunja uhusiano na kisiasa, kibiashara na usafiri na Qatar katikati mwa mwaka 2017, wakiituhumu kwa kuunga mkono ugaidi na kujiweka karibu na adui yao wa kikanda Iran.

Qatar inakanusha tuhuma hizo na inasema mzingiro uliowekewa na mataifa ya Kiarabu unalenga kuudhoofisha uhuru na mamlaka yake.

Qatar iliwahi kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka 2006 lakini Saudi Arabia haijawahi kuandaa mashindano ya OCA. Mwenyeji wa mashindano hayo atatangazwa na mkutano wa baraza kuu la OCA Novemba mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad