Rais Magufuli "Acheni Kusema Kila Anayefariki ni Corona"



Rais Dkt Magufuli amekemea vikali tabia ya baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii, kuhusisha kila kifo kinachotokea na ugonjwa wa #Corona. Rais amesema tabia hiyo inaongeza hofu miongoni mwa wananchi, hivyo amewaagiza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanafuatilia wazushi hao wa mitandaoni na kuwachukulia hatua.

"Kila anayekufa Corona, kila anayekufa Corona, ina maana Malaria imeacha kuua?" Alihoji Rais Dkt Magufuli na kusema ni vyema tabia hiyo ikakoma na taarifa zote za Corona zitatoka kwa mamlaka za Serikali (Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au @wizara_afyatz chini ya @ummymwalimu)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad