Rais Trump anatarajia kutoa uamuzi muhimu katika maisha yake



Kwa mujibu wa rais Donald Trump wa Marekani janga la virusi vya corona linamlazimu kuchukua uamuzi mkubwa kabisa katika maisha yake.

Trump aliwaambia waandishi habari katika Ikulu wa White House uamuzi huo utakuwa muhimu, kuhusiana na lini na vipi nchi hiyo inaweza kurejea katika hali ya kawaida.

Rais Trump alitangaza kuwa siku ya Jumanne atalitangaza jopo la wataalamu, ambao watamshauri juu ya kuirejesha tena nchi hiyo katika hali ya kawaida.

Iwapo muda wa siku 30 uliopo wa kuzuwia watu kutembea utaondolewa, maafisa wa afya wanaeleza kwa mujibu wa gazeti la New York Times, watu hadi 200,000 watafariki kutokana na virusi vya corona.

Marekani imesema leo kuwa ina watu zaidi ya 500,000 walioambukizwa virusi vya Corona.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad